Tuesday, 22 April 2014

JAMII FORUMS (JF): HASAD ZAO

#431   Report Post    
Mohamed Said's Avatar
JF Senior Expert MemberArray
Join Date : 2nd November 2008
Posts : 5,335
Rep Power : 66115Likes Received
3561Likes Given
217

Default Re: Kutoka kofia ya barghashia ya Nyerere 1964 hadi msalaba wa William Lukuvi 2014

Quote By Fundi Mchundo;9326862[SIZE=3Amandla.....
[/SIZE]
Fundi Mchundo,
Ukiwa umeaga sawa hapana neno.

Hiyo ndiyo salama kwako kwani kwa majadiliano hutoweza kunishinda kamwe.

Nilotaka kukueleza naamini umelielewa nalo ni kuwa nalifahamu somo langu
kwa kiwango cha juu sana.

Na wataalamu wa historia ya Afrika wananijua kiasi kuwa mimi ni mmoja wa
waandishi wa Dictionary of African Biographies (DAB) mradi wa Harvard na
Oxford University Press, New York.

Nina uzoefu wa watu kama wewe wa kudharau Waislam.

Katika maisha yangu nimekutana na wengi na wote tumeachana wakiwa na
adabu zao kamili kwangu.

Najua ndani ya moyo wako unakiri ukweli lakini hulka ya binadamu ni kuwa
unajikaza na umeifundisha saikolojia yako kukataa unajiambia, ''Haiwezekani
huyu Mswahili wa Kariakoo...''

Wewe si wa kwanza na hautokuwa wa mwisho In Sha Allah.

Vizuri umeaga.

Nami nakuaga na hii hapa chini:

Mwaka ni 1962.

Mahali ni New Street katika ofisi ya rais wa TANU Nyerere na kabla yake
ilikuwa ofisi ya Abdulwahid Sykes wakati alipokuwa Rais wa TAA 1952/53.

Pamoja na Abdu Sykes na Nyerere yuko Dr. Kleruu.
Wanapanga namna ya kuandika historia ya TANU maana uhuru ushapatikana.

Abdu Sykes kaja na majadala ya baba yake Kleist akiwa katibu muasisi wa
African Association 1929.

Pamoja na nyaraka hizo za baba yake, Abdu Sykes kaja na shajara (diary)
zake binafsi toka 1945 na nyingine kaziandika kwa shorthand (hati mkato).

Zote hizo zinaonyesha harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nyerere kashangazwa na mambo yale...

Hakutegemea kabisa kuikuta historia nzima ya uhuru wa Tanganyika mikononi
mwa Abdu Sykes.

Hakuamini macho yake...
Kapigwa na butwaa kubwa...

Fundi Mchundo,
Ukitaka nikukamilishie kilichotokea nieleze.

Nitakupa kisa kizima kuonyesha jinsi nyoyo zenu zilivyokuwa na hasad na
choyo...

Sishangai na chuki yako dhidi yangu.


Post a Comment