Friday, 5 January 2018

BAHARI ISIYO NA FUKWE: BAADHI YA WANAZUONI WALIOPITA WA ZANZIBAR


[10:28 AM, 1/6/2018] Rijal Hamzah: ASALAAM ALAYKUM!

Siku hizi naanza kufahamu kwanini father alikuwa anapenda kunichukua sehemu mbalimbali kuanzia Skuli, Barazani kwake, Kwenye Nyiradi, Family members kwa kweli imenisaidia sana na father wangu kaishi muda mfupi sana kuanzia 1922 hadi 1969 kati group yake ndio aliokufa mapema.

Hio picha naweza kufahamu baadhi ya watu:

Waliokaa L-R Sh. Harith aliokuwa Mufty wa Zanzibar, Maalim Said Konzi akisomesha Masjid Barza, Syd. Ali Badawy, Syd. Abdul Rahman Sarri,   Syd Omar Abdallah ,  Sheikh Suleiman  Alawy, Syd. Ahmad Hamid Mansab. 

Aliovaa koti aliosimama baina ya Syd Ali Badawy na Syd Abdul Rahman Sarii ni Sheikh Mussa Makungu. Aliosimama nyuma ya Syd Ahmed Hamid Mansab ni Maalim Hakim Saleh Yahya brother wa Prof. Saida Saleh Yahya waliobaki ni wanafunzi.

Huyu Syd Ali Badawy alikuwa kama Visiting Professor akija Zanzibar baina ya Shaaban na Ramadhani.

Lau ingekuwa sio Mapinduzi basi vijana wa kizalendo wengi wangefikia viwango vya juu katika elimu ya dini, kwani wazee wengi wakipenda yaani ''indigenous,'' watoto wao wasome Theology, aidha Msikiti Barza ikipokea watoto wengi kutoka Kondoa Urangi na Malawi kuja kusoma dini na wawili watatu kutoka Afrika ya Kusini.

Sheikh Sleiman alikuwa bahri katika lugha na takriban fani nyingi za ulumu lakini vile vile akitibu majini na mambo ya kiroho na watu wakimsafiria sana. Al Habib Syd Omar bin Sumeyt alimtaka aiwache ''line,'' hiyo na akaiwacha mara moja pasi na kuhoji. Tukizingatia ni kuwa Al Habib Syd Omar bin Sumeyt alimkinga kutokana na kuwa asije akateleza kwa kufanyia watu dawa akadhani labda yupo katika daraja ya juu. Kuna vitu vingi kafanya katika ''spirituality,'' kwa kweli ukisikia utastaajabu na huwezi kuamini.

Safari moja alipambana na Sheikh Abdalla Saleh Farsy wanateremka ngazi za Msikiti Gofu, Sheikh Abdalla akamuuliza hawa majini wanaonekana? Sheikh Sleiman kutaka kumuonyesha Sheikh Abdalla kuwa ana uwezo alimjibu kwa hamaki unataka nikuonyeshe sasa hivi? Sheikh Abdalla alirudi nyuma, haya ananieleza Sharif Abdulwahab wakati tunarudi Darsa tunateremka ngazi akanambia simama, akanambia hii ndio ''point'' ya malumbano ya Sheikh Sleiman na Sheikh Abdalla Saleh Farsy mie nilikuwa nyuma yao, wala sio maneno ya kuambiwa, kwa hio mie itakuwa nimepokea.

Sheikh Sleiman alikuja Dar kwa biashara zake akaja kuumwa na yeye ndio anadarasisha darsa ya Qur'an hapo Masjid Gofu, alipohisi hatoweza muangalie Syd Ahmed Mansab nitakuetea picha yeye na baba yake Syd Hamid Mansab. Sheik Sleiman alimpelekea barua Syd Hamid Mansab apelekewe mkononi na Syd Shibly baba yake Badawy Qulattein, katika barua hio alimtaka adarasishe darsa ya Ramadhani kutokana yeye hatokuwepo na mwanawe huyo aliomo kwenye picha Syd Ahmed Hamid awe ''reserve,'' wake, kwa hio wafanye ''revison'' pamja, akiwa yeye hayupo Syd Ahmed Mansab achukue nafasi na Syd Hamid hajapata kusomesha wala kuhudhuria darsa ya Ramadhani Masjid Gofu kwani akisomesha darsa Masjid Ijumaa Forodhani. Awal Ramadhani baba na mwana wapo kwenye darsa Syd Hamid kadarasisha katikati akaanguka na kufariki hapo hapo, mwanawe Syd Ahmed Hamid aka ''takeover,'' nakuwaeleza watu kuwa siku ya pili darsa inaendelea, jee unapata kitu hapo juu ya Sheikh Sleiman? 

Syd Omar Abdalla ana hikaya refu ambayo nishawahi kuiandika namna alivyotakiwa kuwa Principal wa Muslim Academy.

Father wangu alipokuwa na Syd Omar Abdalla mara zote walikuwa wanazungumza juu ya elimu lakini wakifanyiana maskhara sana ambapo watu wakishindwa kumfanyia maskhara Mwinyi.  Bibi yangu mzaa mama kalelewa kwa kina Mwinyi anasema Mwinyi alikuwa utamuona boza, lakini akishasomeshwa mara moja kila kitu kimekaa na utoto wake akipenda kulala sana, ila haikuwa kama watoto wengine ukilala ndio umelala.

Haya ni machache tunaweza tukayaweka sawa na kuyaingiza kwenye Blog, haya n mazungumzo kuna mengi tutabidi tuyatowe In Shaa Allah.


Post a Comment