Sunday, 11 March 2018

NAKUMBUKA: BARUA YANGU KWA WAZIRI MKUU EDWARD SOKOINE


Edward Sokoine
Jibu langu kwa Ombara:

Chachu Ombara,

Wakati wa ukoloni elimu ilikuwa katika mikono ya serikali na wamishionari na
shule za mishionari zikipewa fungu na serikali kuziendesha kupitia Grant in Aid.
A grant-in-aid is money coming from central government for a specific project. This kind of funding is usually used when the government and parliament have decided that the recipient should be publicly funded but operate with reasonable independence from the state).


Hii ilikuwa kutoka miaka ya 1920 katikati.


Waislam walipoanza na wao kujenga shule zao katika miaka ya 1940 na wao
wakaomba wapewe fungu ili waziendeshe kwa ufanisi kama wamishionari.Serikali ya kikoloni ikakataa kuwaingiza katika Grant in Aid.
Sasa ningependa kukueleza kuwa hapakuwa na Elimu ya Kiarabu.Kilichokuwapo ni elimu ya dini ya Kiislam ambayo hii hadi leo iko katika uhimili
madhubuti wa Waislam wenyewe.Hizi ni madras ambazo wala si lazima maalim awe na jengo anaweza hata kwenye
kibaraza au upenu wa nyumba akasomesha na wanafunzi wakahitimu.Katika miaka ya 1970 wakati wa Nguvu Kazi ya Edward Sokoine walimu wa madras
waliorodheshwa kama watu wasio na kazi.Nataka nikufahamishe kuwa mimi nilimwandikia barua Waziri Mkuu Edward Soloine 
na kumfahamisha kuwa hilo ni kosa hatutafunga madras zetu kwa hiyo Nguvu Ngazi.Nakumbuka katika barua yangu nilimtaja Rashid Kawawa na kuomba asaidie kuileza
historia za madras katika Tanganyika.Barua yangu ilijibiwa na Ofisi ya TANU Lumumba wakiniomba nifike ofisini kwao ili
wanieleweshe.Jibu nililowarejeshea lilikuwa wa kuelimishwa si mimi bali ni Waislam ndiyo waelezwe
tatizo liko wapi.Sikupata jibu lakini madras zikaendelea hadi hii leo na hakuna mwalimu yeyote wa
madras alikamatwa katika operesheni ya Nguvu Kazi.
Post a Comment