Showing posts with label gallery. Show all posts
Showing posts with label gallery. Show all posts

Tuesday, 13 January 2015

Kipindi Maalum Radio Kheri '' Sheikh Ali Muhsin Barwani (1919 - 2006)


Msomi, Mwanasiasa, Mshairi, Mhariri wa Gazeti, Mwandishi wa Vitabu, Mwalimu na Mfasiri wa Qur’an Tukufu
Kumbukumbu yaMiaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar'' 

Chini Kwenye Ngazi ya Ndege Ali Muhsin Barwani, Mohamed Shamte,
Hasnu Makame na Abeid Amani Karume

Sheikh Ali Muhsin Barwani wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar alikuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP) vilevile chama hiki kikijulikana kama Hizbu. Kwa mapenzi makubwa wanachama wa Zanzibar walikuwa wanamwita, “Zaim” yaani Kiongozi. Ilikuwa nia ya Sheikh Ali Muhsin Zanzibar ipiganie uhuru wake chini ya chama kimoja cha kizalendo chenye nguvu chama cha kitaifa badala ya vyama vilivyojijenga katika misingi ya rangi. Ilikuwa pigo kubwa sana kwake Abeid Amani Karume alipoasisi Afro Shirazi Party, chama kilichosimama kwa maslahi ya Waafrika na Washirazi. Sheikh Ali Muhsin alipigania uhuru wa Zanzibar mpaka ukapatikana tarehe 10 December 1963. Sheikh Ali Muhsin alishiriki katika mkutano wa katiba Lancaster House. Baada ya mapinduzi yaliyotokea Zanzibar tarehe 12 Januari 1964 Sheikh Ali Muhsin alikamatwa na kusafirishwa Tanganyika ambako alifungwa Ukonga na jela nyingine kwa kipindi cha miaka 10 na miezi michache. Katika kipindi alichokuwa kifungoni Sheikh Ali Muhsin aliandika miswada kadhaa ambayo alikuja kuichapa kama vitabu baada ya kutoka kifungoni. Kabla hajafa mwaka 2006 Sheikh Ali Muhsin aliandika kitabu cha maisha yake, ‘’Conflict and Harmony in Zanzibar,’’ ambacho kilikuja kufasiriwa  kama ‘’Kujenga na Kubomolewa Zanzibar.‘’ Katika kitabu hiki cha maisha yake Sheikh Ali Muhsin anaeleza yaliyopitika Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi. Baada ya kushindwa kupata pasi ya kusafiria, Sheikh Ali Muhsin alitoroka nchini mwaka 1974. Hadi anafariki siku zote Sheikh Ali Muhsin alikuwa akisema yale hayakuwa mapinduzi bali mavamizi.

Mwandishi Akisoma Kutoka Kumbukumbu za Sheikh Ali Muhsin Barwani

Studio za Radio Kheri Kipindi Maalum Cha Mapinduzi ya Zanzibar

Studio za Azam TV Kipindi Maalum Cha Mapinduzi ya Zanzibar


Monday, 19 May 2014

Tuesday, 13 May 2014

Mohamed Said

Sikiliza Kipindi Maalum cha Sheikh Ilunga Hassan Kapungu Radio Kheri (Dar) na Radio Quiblaten (Iringa) na Kumbukumbu aliyofanyiwa Msikiti wa Mtambani

Mzungumzaji Katika Kipindi cha Redio ni Mohamed Said akihojiwa na Butije Khamis

Ingia:
 www.mohammedsaid.com

Butije Khamis

Friday, 9 May 2014

Sheikh Ilunga Hassan Kapungu

Video Kumbukumbu ya Sheikh Ilunga Hassan Kapungu
Msikiti wa Mtambani Ijumaa 9 May 2014
Radio Kheri 104.10 FM Dar es Salaam na Radio Quiblatein Iringa leo Ijumaa 9 May watarusha kipindi maalum ''Kumbukumbu ya Sheikh Ilunga Hassan Kapungu (1957 - 2014).''  Kipindi kitarushwa 21.30 HRS (saa tatu unusu ya usiku saa za Afrika ya Mashariki). 

Walio nje ya Dar es Salaam wanaweza kupata radio zote mbili katika radiostationstz.com.

Ndani ya Studio za Radio Kheri 104.10 FM Faraja Kwa Umma
Kumbukumbu ya Sheikh Ilunga Hassan Kapungu
Mtangazaji Butije Khamis Akishirikiana na Radio Qublaten Iringa Akiendesha Kipindi Maalum:
Kumbukumbu ya Sheikh Ilunga Hassan Kapungu


Butije Khamis Akiendesha Kipindi Maalum Kuhusu
Kumbukumbu ya Sheikh Ilunga Hassan Kapungu

Tutaweka Audio ya Kipindi In Sha Allah...
Sikiliza hapo chini bofya: 

Thursday, 8 May 2014

Kipindi cha Jukwaa kwa Asiye na Jukwaa, Kilichofanyika Radio Kheri Dar es Salaam 27 April 2014