Showing posts with label makala. Show all posts
Showing posts with label makala. Show all posts

Sunday, 19 November 2017

Utangulizi
Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ni kijana hodari mwenye kujua kuchagua maneno yake vyema. Hapo chini ameandika masikitiko yake kuhusu Tanzania kukataa kupiga kura kulaani mauaji ya Waislam Myanmar. Katika maandishi yake neno, ''Waislam,'' halipo. Lakini dunia nzima inajua kuwa wanaouliwa Myanmar ni Waislam si suala la kuuliwa ''wananchi.'' 

Iwe itakavyokuwa Zitto Kabwe kaeleza masikitiko yake ili Watanzania wajue nini kimetokea. Kwa sera ya Tanzania kuhusu msimamo wake wa kusimamia haki duniani kote kitendo haya ni mabadiliko makubwa sana katika msimamo huo uliowafikisha Watanzania kupigana Msumbiji bega kwa bega na Frelimo na kutoa misaada kote kulikokuwa na dhulma sawa na kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliposema, ''Tunataka kuwasha mwenge uangaze kote na kuleta matumaini kule watu walikokata tamaa.''

Hii sera mpya ya kushindwa kulaani mauaji ya Waislam wanaouliwa Myanmar huenda hii ikawa ni sera mpya ambayo kwa sasa ndiyo inaongoza Tanzania na uhusiano wake na mataifa mengine. Ndiyo kusema kuwa sasa Tanzania haijali tena dhulma bali inaongozwa na maslahi yake mengine ambayo kwa bahati mbaya kwa sasa hayajakuwa bayana. 

Tanzania ilianza na kurejesha uhusiano na Israel uliovunjwa na Baba wa Taifa mwenyewe nusu karne iliyopita. 

Leo Tanzania imeridhia kutopiga kura kwenye mauaji ya kimbari ya Waislam wa Mynmar. 

Wachunguzi wa siasa wanasubiri kutazama nini lingine litafuatia. Labda hilo litatoa mwanga zaidi kuonyesha nchi yetu imesimama upande gani na kwa nini. 

Swali la kujiuliza ni hili: Ingekuwa ni kura ya East Timor na wanaouliwa ni Wakatoliki Tanzania ingekaa pembeni ikaacha kupiga kura?

Jibu unalo wewe ndugu msomaji wangu.Unaweza kusoma historia ya Tanganyika na Palestine hapo chini:
http://www.mohammedsaid.com/2017/06/baada-ya-kuondoka-baba-wa-taifa.html

Tanzania yalaumiwa vikali kwa kutopigia kura azimio la UN la kutetea Waislamu wa Myanmar


http://parstoday.com/sw/news/africa-i36555-

Tanzania_yalaumiwa_vikali_kwa_kutopigia_kura_azimio_la_un_la_kutetea_waislamu_wa_Myanmar
Mbunge mashuhuri katika bunge la Tanzania ameikosoa vikali serikali ya nchi hiyo kwa hatua yake ya kutopigia kura azimio la Umoja wa Mataifa linalotaka serikali ya Myanmar ikomeshe operesheni za kijeshi zinazolenga kukandamiza jamii ya wachache ya Waislamu Warohingya nchini humo.

Siku ya Alkhamisi iliyopita Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu ilipitisha rasimu ya azimio linaloitaka serikali ya Myanmar ikomeshe operesheni za kijeshi ambazo "zimesababisha ukiukaji ulioratibiwa na uvunjaji wa haki za binadamu" za Waislamu Warohingya wanaoishi katika jimbo la Rakhine.

Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 135 zilizounga mkono, nchi 10 zililipinga na nyengine 26 ziliamua kutopiga kura, Tanzania ikiwa moja ya nchi hizo.

Zitto Kabwe akiamkiana na Rais John Magufuli (aliyevaa miwani) 


Akiandika katika ukurasa wake wa kijamii wa Facebook, Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo, amesema: "Juzi Umoja wa Mataifa kulikuwa na kura ya Azimio la kulaani vitendo vya unyama dhidi ya watu wa kabila la Rohingya huko Myanmar. Nchi yetu haikupiga kura (abstained). Ni kitendo cha aibu sana Tanzania kushindwa kulaani vitendo vya namna hii".

Msimamo huo wa Tanzania umetafsiriwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kidini wa nchi hiyo kama kielelezo cha kubadilika sera za serikali ya sasa ya Dar es Salaam katika suala la kutetea haki na uadilifu duniani.


Balozi wa Tanzania Israel Job Masima akikabidhi hati zake za utambulisho kwa Rais wa utawala huo wa Kizayuni Reuven Rivlin

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni serikali ya Tanzania ilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel. Na hii ni katika hali ambayo msimamo wa huko nyuma wa Tanzania tangu enzi za uongozi wa Rais wa kwanza wa nchi hiyo hayati Mwalimu wa Julius Nyerere ulikuwa ni wa kutetea harakati za ukombozi za wananchi wa Palestina katika kukabiliana na dhulma na ukaliaji mabavu wa ardhi zao unaofanywa na utawala haramu wa Israel.../

Sunday, 15 October 2017


Enzi za Ulaya ya Kale (Medieval Europe) kulikuwa na watu katika mabaraza ya wafalme kazi yao kubwa ilikuwa kumstarehesha mfalme kwa kumchekesha na katika kufanya hivyo kulichekesha barza zima. 

Wachekeshaji hawa walikuwa wanaitwa, ‘’Court Jesters.’’ 
Hawa walikuwa wachekeshaji tu na wakiendesha maisha yao kwa kazi hiyo ya kuchekesha. 

Kujipambanua walikuwa wana mavazi yao maalum ya kazi yao hiyo. 

Kama ilivyo kazi yao walioajiriwa walikuwa pia na mavazi yanayoendana na taaluma hiyo nayo ni mavazi ukiyaangalia tu mwenyewe unacheka. 

Nimeweka picha hapo chini kumwonyesha mchekeshaji wa mfalme alikuwa anaonekanaje. 
Court Jester alikuwa hana madhara katika jamii ukiacha ile kuwaumiza watu mbavu kwa kucheka.Mchekeshaji katika Barza ya Mfalme
(Court Jester)Lakini siku hizi pia wapo Wachekeshaji wa Mfalme, yaani, ''Court Jesters.''

Hawa kwa kuwa  dunia hii ya leo hakuna tena Barza za Wafalme utawakuta katika vyama vya siasa wakijikomba kwa wakubwa. 

Humo ndani ya vyama vya siasa ndimo walikojenga mabarza yao siyo ya uchekehaji bali ya fitna. 
Hawa hawachekesheshi watu bali hawa wanawafurahisha baadhi ya viongozi kwa namna ya kipekee.

''Court Jesters,'' hawa kazi yao kubwa ni kuwashambulia kwa maneno makali wale ambao wanaonekana wako dhidi ya ‘’Mfalme,’’ kwa kutumwa au wakati mwingine kwa kujituma wenyewe.

''Court Jesters,'' wa kale kazi yao ilikuwa ni kuchekesha hawa wa leo kazi yao ni kuumiza hisia za watu kwa maneno yanayochonganisha na kuvunja misingi ya umoja na utangamano. 

Kazi hii kwa hakika ukifanya uchunguzi wa kuwaangalia, ''Court Jesters,'' waliopita utagundua kuwa inahitaji mtu kuwa kidogo umepungukiwa katika uwezo wa fikra. 

Wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika kulikuwa na Rashid Sisso lakini huyu hakumdhuru mtu kazi yake ilikuwa kumchangamsha Nyerere katika mikutano ya hadhara na kwa kufanya hivyo kuiamsha hadhira pia isikize nini TANU inasema kama ujumbe kwa wananchi.

Hawa, Court Jesters wa leo hawako hivyo wameelemewa katika fitna na ili uiweze kazi hii sharti moja ni kuwa uwe hodari katika somo la farka.

Vinginevyo kazi hutaiweza. 
Itakushinda

Hii ni mfano wa yule mtu mfupi katika, ‘’circus’’ yaani, ‘’midget,’’ Kiswahili anaitwa, ''kibushuti.''
Ili uweze kuwa, ‘’midget,’’ katika, ‘’circus,’’ lazima uwe huna kimo, uwe kajitu kafupi na kadogo - kibushuti. 

La imetokea ulikuwa, ‘’midget,’’ kisha kwa rehma za Allah ukajaaliwa kuwa na urefu wa mtu wa kawaida mwenye, ‘’circus,’’ yake atakufuta kazi kwa kuwa huna tena ile sifa ya kuwa kichekesho.

Utakuwa umepoteza mvuto kwa watazamaji kwani wewe si kibushuti tena.
Angalia hiyo picha hapo juu. 

Huyu bwana kaalikwa katika hafla ya kutembelea meli kutoka Oman iliyokuja kupalilia udugu baina ya wananchi wa Oman na Zanzibar. 

Labda kuwa kuogoapa asije akawa kama ‘’midget,’’ aliyerudi kuwa mtu wa kawaida akaona ni muhimu kunigia katika meli hiyo akiwa katika mavazi yake anapokuwa kilingeni akistarehesha, na kumburudisha mfalme. 

Kaingia melini kavaa mavazi yake ya kazi.

Kawavalia waliomwalika kanzu yenye rangi ya chama chake.
Aliona ule ni uwanja stahiki wa kufikisha ujumbe wake. pale.

Wakubwa zake wanaipeleka saa mbele yeye kashika mishale anairudisha nyuma tena kwa kuipiga nyundo nzito.

Hakika huyu ni  Mchekeshaji wa Mfalme, ''Court Jester,'' katika ubora wake.

Midget
(Kibushuti)

Saturday, 14 October 2017

Sheikh Ponda akiwa Mahakamani Morogoro yuko kizimbani akizungumza
na Wakili Juma Nassoro


kipara kipyaJF-Expert Member

#1
Today at 7:44 AM
Joined: May 2, 2016
Messages: 2,321
 
Likes Received: 1,845
 
Trophy Points: 280

Sheikh Ponda ni muda mrefu anajulikana kama mwanaharakati na kiongozi wa kupigania mali za waislamu,Ponda ana historia ndefu na amepatwa na misukosuko mingi katika kuendesha harakati zake na wengi walijitokeza kumtetea kwa sababu ya kuvaa kofia ya kuonyesha kuwa anatetea imani fulani,lakini hili linalotokea sasa ni dhahiri sasa Ponda anajipambanua kuwa ni mwanasiasa na yupo tayari kisiasa na tumkaribishe rasmi katika ulingo wa siasa na asihukumiwe kidini aonekane ni mwanasiasa kama wengine tu

Ponda asiogope mbona dkt Slaa alikuwa ni askofu akaamua moja,mchungaji Msigwa na bado wanafanya siasa za uwazi bila ya kujificha kwenye kivuli cha dini.

Ponda hukuzungumzia msikitini habari zako umezungumzia ukumbini,wakili ni Safari makamu mwenyekiti CHADEMA hivyo umekamatwa kama mwanachadema.

Pesa ya chadema haikuwahi kuwaacha watu salama

Ponda umevalishwa mkenge!

Siasa mpaka 2020!

New
Aksante sana mkongwe mohamedi saidi kwa mchango wako hoja yangu ipo hapa ndio maana nimesema wasije wakampa kesi ya udini kwa maana ya kuambiwa ni gaidi,ila achukuliwe kama mwanasiasa maana ukiwa mwanasiasa upo huru kusema chochote, ukiwa sheikh na ukauvaa usiasa muda wowote unaweza kuwa katika orodha ya magaidi!

 Kipara...
Toka zimeanza kesi za ugaidi hakuna hata kesi moja sheikh yeyote
amekutwa ha hatia ya ugaidi huu sasa mwaka wa 15.

Kesi mashuhuri ya masheikh wa Uamsho huu mwaka wa 4 ushahidi
bado haujapatikana kuwatia hatiani kwa ugaidi.

Ama kuhusu suala la udini ikiwa Sheikh Ponda atashtakiwa kwa hilo
sijui itakuwa katika kipengele gani cha sheria.

Lakini hebu tujaaiie kuwa atashitakiwa kwa kosa la, ''udini,'' basi hiyo
itakuwa kesi ya karne na mengi ambayo hayajasemwa hadharani hapo
yatasikika mahakamani Sheikh Ponda atakaposimama kujitetea.

Thursday, 28 September 2017
Utangulizi
Imekuwa jambo la kawaida kwa Maalim Seif kutukanwa a kukebehiwa katika mitandao ya kijamii na watu ambao wanafahamika. Binafsi siku za mwanzo nilijaribu kuwa naandika nasaha kujaribu kuwafahamisha wahusika wa kejeli na matusi kuwa huyu wanaemvunjia heshima ni kiongozi mkubwa katika nchi yetu lakini ilibidi niache kwa kuona kuwa hawakuwa tayari kunisikiliza na zaidi matusi na kejeli zikizidi. Lakini kinachonistaajabisha  vipi vyombo husika kuwa kimya.
MS

Kuna wakati sasa inakaribia miaka 20 watu fulani walinifikiria kuwa nina, ‘’ujuzi,’’ ambao ungekuwa na manufaa katika taifa letu na baadhi ya watu hao ni wakubwa wakataka nikautumie, ‘’ujuzi,’’ huo wangu katika ofisi kubwa sana ya serikali.

Kipindi hiki ni kile kipindi ambacho palikuwa na malalamiko mengi kuwa kuna upogo mkubwa katika kushika madaraka katika serikali kuwa jamii moja fulani imeachiwa kuhodhi serikali nami nilikuwa mmoja wa watu wenye fikra hizo.

Katika walikuwa wametumwa kunishawishi nikubali ombi hili la kwenda kuitumikia serikali yetu ni mwalimu wangu wa Chuo Kikuu ambae yeye tayari alikuwa serikalini na ameshika nafasi kubwa.

Lakini ukweli ni kuwa hii kwangu mie lilikuwa, ombi  la pili, ombi la kwanza lilikuwa niingizwe chamani  kabisa.

Kweli nilistaajabu kwa mtu mdogo kama mie kuonekana kuwa naweza kuwa na manufaa katika utendaji wa ufanisi katika nchi yangu.

Hili pendekezo la utumishi chamani nilimwambia mjumbe na sahib yangu aliyenifuata kuwa akili yangu jinsi ilivyo sitaweza kukamilisha majukumu nitakayopewa kwa ufanisi na kubwa nililohofia ni kuwa vipi nitawatazama ndugu zangu machoni?

Nitaingia msikiti gani kuswali bila kuingiwa na simanzi?
Huu ndiyo ukawa mwisho wa jambo lenyewe.

Hili la pili sikuweza kukataa hapo kwa hapo kwa sababu fulani fulani kwa hiyo nilipeleka hadi CV yangu.

Lakini katika nafsi yangu niliamini kabisa kuwa hili haliwezi kuwa kwani mimi nimefika mbali sana na kukanyaga ardhi ambayo wengi kabla yangu na wajuzi kunishinda hawakuthubutu kutia mguu wao.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa baada ya muda siku moja nikapigiwa simu ya dharura nikiendesha gari nikaambiwa haraka nirudi ofisini kwangu nitume tena ile CV yangu mara moja kwani ile ya kwanza haionekani.

Nilitii.

Lakini nilijuwa kuwa hili haliwezekani na kweli hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Bahati nzuri au mbaya hata kama yangefanikiwa sidhani kama ningedumu kazini.

Allah hakunijaaliwa ustahamilivu kuacha kusema kile ninachoakiamini kuwa kweli.

Wazee wangu wawili Allah awarehemu, Ally Sykes na Kitwana Kondo wote wakinipenda na wote walipatapo kunambia kwa huruma sana kuwa nitakufa masikini na Mzee Ally alikwenda mbali zaidi alinambia, ‘’Mohamed utakufa masikini kama baba yako Allah kakujaalia vipaji lakini umeshindwa kuvitumia…’’

Bwana Ally alipomaliza kusema maneno haya akaniuliza umri wangu. Nilikuwa na miaka 40.
Ally Sykes akatingisha kichwa kwa masikitiko.

Mzee Kondo yeye alinifananisha na wenzangu wa rika langu na wengine ni marafiki zangu akamwambia mkewe, ‘’Mwanangu huyu ndiye pekee dunia yake haikumkalia vizuri.’’

Nimeleta utangulizi huu kwa kuona imewekwa picha hapa ikimkebehi mmoja wa viongozi wa nchi yetu.

Nimeona na mie nichangie katika hiyo picha lakini kwa kuweka staha kuwa iko siku iliwekwa picha mfano wa hii lakini mimi nilipochangia nikaonywa kuwa nisifanye hivyo nami nikatii na kuomba radhi nikasema kwa kuwa nimeona picha hiyo imewekwa mwekaji na kaandika maneno hakukemewa nikadhani inaruhusiwa.

Mradi kumbe ni makosa naomba radhi mnisamehe.

Sasa katika hili lililo mezani wengi wameona hiyo picha lakini wamekaa kimya kwa nini  mimi?
Lugha ya sasa unaweza kusema kwanini ‘’nimewashwa?’’

Rejea katika utangulizi wangu jibu liko hapo.

Bibi zangu wake zangu mabinti Farijala wakisema, ‘’Masikini mume wetu Mohamed, ule ‘’wazimu,’’ wote wa babu yake Mzee Popo wanae wote umewaruka umekuja kumvaa mjukuu wake.’’

Mie huwaambia watu kuwa Wamanyema wote wewe tuchungiuze tuna wazimu kidogo.
Baba Juma atanisaidia kusadikisha.

Sunday, 6 August 2017Mubindi,
Suala la takwimu nchi petu baina ya Waislam na Wakristo ni jambo nyeti
sana na kwa hakika Afrika yote hili ni jambo linaloleta ubishani mkubwa
sana.

Wakati naandika kitabu cha Abdul Sykes ilifika mahali lazima hili suala
nilizungumze.

Naweka hapo chini kile nilichosema:

''According to the 1957 population census, Muslims outnumbered Christians at a ratio of three to two. This, at that time, meant that Tanzania was a leading Muslim nation South of the Sahara. But in the first post-independence census of 1967 the total figures for Tanzania Mainland were 32% Christian, 30% Muslim and 37% local belief (August H. Nimtz Jr, Islam and Politics in East Africa, University of Minneapolis, 1980, p.11). These figures show Pagans as a leading majority in Tanzania. The 1967 census has not been able to show the reasons for the sudden decrease of Muslim population nor the growth of animists amidst believers in the span of the last ten years.

This was the last population census showing religious distribution.

Unfortunately power sharing in the political system in Tanzania is very much skewed against Muslims, although it is known that the stability of any nation depends on proper balancing of these facts. Different sources provide different Muslim -Christian religious distribution figures. These conflicting figures are as a result of sensitivity of the issue. Among African countries with sizable population of Muslims and Christians, like Tanzania and Nigeria,[1] the inquiry as to which faith commands a leading majority, is a source of potential conflict and controversy. Tanzania is of no exception. D.B. Barret[2]gives figures which show Muslims as a minority in Tanzania. The Muslim population is purported to be 26%, Christian 45%, local belief 28%. Tanzania National Demographic Survey figures for 1973 put Muslims in Tanzania slightly above Christians at 40%, Christians 38.9% and local belief 21.1%. But according to Africa South of The Sahara, [3] Muslims in Tanzania are a leading majority at 60%. This figure has remained constant in all its publications since 1982. Since research by Tanzanian Muslims on Islam is scant or almost non-existent, the issue of Muslim population has yet to be tackled from an Islamic point of view. [4]

Distribution of authority and power sharing is a factor which should not have been a cause of conflict in independent African countries. Ironically this has become a point of controversy only under indigenous governments.

It is a sensitive issue because ethnicity, religious identity and clanship is an important factor in independent African states. Power distribution and numerical strength has also to be reflected in the sharing of political power along those lines.

During colonial rule, distribution of power under ethnicity and religious bias in Africa by colonising powers were not perceived as so serious a breach of trust by subjects as to warrant civil upheavals.

Fortunately tribalism is not pronounced in Tanzania, but religion has been a factor of discrimination since colonial days.''

[1] Ali A. Mazrui, ‘African Islam and Competitive Religion: Between Revivalism and Expansion’, in Third World Quarterly Vol. 10. No. 2 April, 1988, pp. 499-518.
[2] D.B.Barret, Frontier Situations for Evangelisation in Africa ,Nairobi, 1976.
[3] Africa South of The Sahara, Europa Publication, London, No. 20, 1991, p. 1027.
[4]The only conclusive Muslim research is by Dar es Salaam University Muslim Trustee (DUMT), see 'The Position of Muslims and Islam in Tanzania', in Al Haq International (Karachi) September/October 1992.

Bahati mbaya nimeandika haya katika Kiingereza lakini tunaweza tukafanya mjadala kwa Kiswahili.

Katika hayo niliyoweka hapo juu nimefuta kipengele kimoja kinachosema kuwa takwimu za sensa ya mwisho iliyokuwa na kipengele cha dini ''zilichezewa.''

Nimekifuta makusudi kwa kuwa ingawa ipo ''citation,'' nina hakika kitasababisha mapambano makali hapa jamvini.

Sasa turudi latika hizi takwimu za CIA.

Nilikuwa nafanya mhadhara Chuo Kikuu Cha Iowa, Marekani kuhusu ''Uislam
na Siasa Tanzania Historia ya TANU na Uhuru wa Tanganyika.''

Katika mhadhara ule nilieleza sababu za Waislam katika takriban miaka 20
iliyopita kuwa na maandamano na mapambano ya mara kwa mara na serikali.

Nikaeleza sababu kuu ni kuwa Waislam wamekuwa pembeni katika elimu na
hivyo kuwa pembeni katika kugawana madaraka ya kuendesha nchi.

Waislam walitaka hili liangaliwe na serikali kwani ipo harufu ya hujuma.

Katika kipindi cha maswali na majibu na ilipobaki kama dakika tatu hivi nihitimishe,
ndipo likaja swali hili lililokuwa na takwimu za CIA na muulizaji alikuwa profesa wa
historia akasema kuwa wakipatacho Waislam wa Tanzania hiyo ndiyo haki yao kwa
kuwa wao ni wachache, yaani ni ''minority.''

Hili swali naamini liliwekwa hadi mwisho kwa kuwa katika mazungumzo yale walitaabika sana ni historia ya uhuru niliyokuwa nawafunulia, historia ya wazalendo Waislam katika kupambana na ukoloni, historia ambayo kwao wao ilikuwa ngeni.

Wao walizoea mihadhara ya kuja na historia rasmi iliyomtaja Mwalimu Nyerere 
peke yake kuwa ndiyo aliyoikomboa Tanganyika kutoka kwa Waingereza.

Hawakutaka nitoke pale kichwa juu kifua mbele walitaka wanifedheheshe kwa hizi
takwimu za CIA zinazonyesha kuwa Tanzania ina Waislam wachache na mambo
yote ni shwari ila kwa vurugu hizi za, ''Waislam wa siasa kali.''

Historia yangu ilikuwa imewahuzunisha.

Katika hadhira ile alikuwapo Prof. James Giblin aliyafanya utafiti na kuandika kitabu
kuhusu Vita Vya Maji Maji.

Alikuwapo pia Prof. Michael Lofchie aliyeandika kitabu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar, ''Revolution in Zanzibar,'' na hawa wote wameishi Tanzania na wanaijua vyema.

[​IMG]
Prof. Michael Lofchie

[​IMG]
Prof. James Giblin

Jibu langu kwao halikuwa kwangu mimi kugonganisha takwimu zangu kama zilivyo
katika kitabu cha Abdul Sykes, na takwimu zao za CIA, la hasha.

Mimi nilijibu swali lao kwa kuwauliza wao swali.

Niliwaambia kuwa naomba wanionyeshe nchi yoyote duniani katika historia yao
wananchi walio pungufu yaani, ''minority,'' walionyanyuka na silaha mikononi
kupambana na taifa lililoingia katika nchi yao kwa nia ya kuwatawala.

Nikawarejesha katika hitoria ya Vita Vya Maji Maji na kuwaambia wafanye rejea
na waangalie ni nani waliunda majeshi ya kupambana na Wajerumani.

Nikawakumbusha kisa cha Sultani Abdulrauf Songea Mbano wa Wangoni
alivyonyongwa na Wajerumani kwa kuongoza vita dhidi yao.

Nikawaambia wafanye tena rejea waangalie harakati za siasa za uhuru zilipoanza
baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 - 1945) ni nani walikuwa mstari wa mbele
katika, ''nationalist politics,'' Tanganyika?

Kweli inawezekana adui aingie katika nchi bila ya ridhaa ya wenye nchi na ikawa
walionyanyuka kupinga uvamizi huu wakawa ni wale, ''minority?''

''Majority,'' ya wenye nchi wako wako wapi hadi mapambano ya kuikomboa nchi iwe
mikononi kwa ''minority,'' na katika Tanganyika iwe Waislamu?

Ukumbi wote ulikuwa kimya.

Maprofesa wa historia ya Afrika walikuwa wanajaribu bila shaka kutafuta mfano
utakaoweza kupambana na hoja yangu.

Hawakuweza kuupata.

Nchi zote duniani mapambano ya ukombozi huongozwa na wale waliokuwa, ''majority.''

Nikamaliza kwa kusema kuwa sina ugomvi na takwimu za CIA lakini Waislam wa
Tanzania wanaujua ukweli.

Palepale Jonathon Glassman bingwa wa African History kutoka Northwestern University,
Evanston Chicago akaniomba niende chuoni kwake tukafanye madahalo kama ule
tuliofanya pale Universty of Iowa.

Glassman amekaa sana Pangani na Tanga mjini wakati anafanya utafiti wake na
kaandika kitabu ''Feats and Riots,'' anaijua vizuri Tanzania.

Nilikubali mwaliko na nilizungumza Northwestern University, Ukumbi wa Eduardo
Mondlane
.


Monday, 24 July 2017


Riziki Shahari: Mamlaka ya Bunge kikatiba siyaoni


Rate This

UKIJUA historia ya ujanani kwake alivyokuwa akisoma hadi alipohitimu elimu ya kidato cha tano katika Shule ya Wasichana ya Korogwe mwaka 1980, ndio utaelewa ni kwa nini leo Riziki Shahari Mngwali ametokea kuwa mwanamke mkakamavu asiyeyumba kimsimamo.
Nimebaini kuwa hivyo ndivyo alivyo Bi Riziki, mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) na mbunge wa Viti Maalum.
Mama huyu, mzaliwa wa mwaka 1960, ni kiongozi shupavu aliyejijengea heshima kubwa tangu akiwa katika Bunge Maalum la Katiba (BMK) lililodumu kwa miaka miwili kuanzia mwaka 2013 mpaka 2014.
Bi Riziki ni mwingi wa maelezo yenye maneno mazito ambayo huachi kufikiri mara mbili ukiyasikia. Wala hana muhali akijisikia kusema.
Akiipata nafasi ya kusema jambo analolijua na kuliamini, husema hasa. Hafichi kitu na hana sababu ya kudanganya. Huwa anajitoa na kusema ukweli mtupu kinagaubaga.
Katika mahojiano mahsusi na MwanaHALISI yaliyofanyika Jumatano wiki iliyopita kwenye ofisi ya wabunge wa CUF jijini Dar es Salaam, mbunge huyo anasema ukakamavu wake ni wa asili tangu akiwa shule.
Anakumbuka visa mkasa vitatu vilivyomsukuma kuingia kwenye siasa. Mosi, anasema wakati akisoma kidato cha tano na sita katika shule ya wasichana Korogwe ya mkoani Tanga, walifundishwa somo la siasa iliyoelekeza namna ya kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pia jioni walipata mafunzo ya siasa ya lazima kutoka CCM yaliyojumuisha hata wale wanafunzi ambao hawakupangwa kusoma somo la siasa.
“Sikuona umuhimu wa kurudia kufundishwa kitu kimoja mara mbili. Nilihoji kuhusu hili na wakati wa mahafali ya kidato cha sita tukalazimishwa kufanyiwa sherehe pamoja na waliosoma mafunzo kuhusu CCM ambao hawakuwa wahitimu.
“Tulipohoji, tukanyimwa kadi ya uanachama ya CCM,” anasema Riziki.
Kadi hiyo anasema ndiyo iliyotumika kama kiambatanisho cha kujiunga na chuo kikuu na hata mafunzo ya kijeshi jambo amabalo anasema lilikuwa linawanyima haki ya kupata elimu kwa sababu tu ya kukosa kadi.
Kisa cha pili, anasema, ni wakati akituma maombi ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, katika fomu za maombi ilitakiwa pia maelezo ya wajumbe wa CCM wa mtaa alioishi kuhusu ushiriki wake katika kujenga chama.
“Basi mama yangu akachukua zile karatasi na kuzipeleka kwa wajumbe. Wale wajumbe wakata niende mwenyewe. Mama akawambia kwa kuwa wananifahamu fika wangeweza tu kunijazia bila ya mimi kuwepo; wakagoma kujaza, nikashindwa kutuma maombi, badala yake nikaomba nafasi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nikapata,” anaeleza Riziki.
Je, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hakukuhitajika maelezo ya wajumbe wa shina wa CCM? Anasema, “Chuo Kikuu Dar es Salaam sikupata shida, wao walitaka tu kadi ya CCM ambayo nilikuwa nayo.”
Kisa cha tatu ni kilichomhusisha kada wa CCM. Alikuwa kiongozi ila hana uhakika ni ngazi ipi lakini anahisi alitoka wilayani. Anamkumbuka kuwa na kiburi. Alifika shuleni kwao Korogwe na kuitisha mkutano na kuanza kuwatisha.
Anasema kiongozi huyo aliwatisha kwamba angewaweka ndani kama wangehoji chochote kuhusu utawala au serikali na akawapa mfano namna alivyomweka ndani kijana mmoja baada ya kuhoji kwa nini walilazimishwa kusema “zidumu fikra za Mwalimu Nyerere.”
Kijana huyo alisema kwa mujibu wa Kiswahili fasaha, si sahihi kusema “zidumu fikra za Mwalimu Nyerere” wakati mwalimu alikuwa bado hai. Kauli hiyo ingefaa kutumika kama mwalimu angekuwa amekufa. Akaswekwa ndani.
“Hivi visa vitatu vilitosha kunifanya kuuchukia utawala wa CCM kwa kuwa niliona haukutoa uhuru. Ulikuwa kandamizi… nilitamani siku moja niingie kwenye siasa nitetee haki hata kama nisingekuwa kiongozi katika siasa,” anasema Riziki.
Kwa sasa Riziki ni mbunge, nafasi aliyoipata katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kupitia utaratibu uliowekwa na chama chake. Japo si mara yake ya kwanza kuwania nafasi hiyo. Mwaka 2005 aliomba lakini hakubahatika.
Anasema matarajio yake na anachokiona bungeni ni tofauti. Anavyoamini, uhuru na demokrasia pana ni muhimu ili nchi kufikia maendeleo.
Anasema “niliingia bungeni kwa hamu kweli nikidhani ni chombo kikubwa kinachowakilisha wananchi na kinachofanya maamuzi kwa kujitegemea. Lakini ni tofauti.”
“Nilitarajia sisi wabunge ni wawakilishi wa wananchi na wasimamizi wa serikali. Yale mamlaka ya kikatiba ya Bunge siyaoni katika bunge hili,” anasema.
Anatoa mfano kuwa wabunge wa upinzani wanapoihoji serikali au kuishauri, mara nyingi wanazuiwa. “Kiti cha spika au wabunge wa CCM wanatumika kuitetea serikali. Sio wajibu wao,” anaeleza Riziki.
Mbali na Bunge kutumika kama wakala wa serikali, Riziki anaona mbunge mmoja mmoja hapewi hadhi inayotakiwa kama mwakilishi wa mamilioni ya wananchi. Badala yake, hata hukumu dhidi yake zinatolewa kama mtu binafsi.
“Lakini bado sijakata tamaa. Vichwa makini vya wapinzani vilivyopo mle ndani (bungeni) vinanitia moyo. Hata wananchi nao wananitia moyo. Wanaelewa kila kitu kinachoendelea bungeni. Si wajinga,” anasema.
Akieleza hali ya demokrasia nchini, anasema “Ni mbaya. Huwezi kuwa na demokrasia bila ya kuruhusu midomo kuzungumza. Kinachofanyika sasa ni hofu, na makatazo ndiyo yametanda. Siasa ni maisha ya kila siku. Hakuna kipindi maalum cha kufanya siasa.”
Anasema utendaji wa serikali si mzuri. Unaweza kuwa na nia na mambo mazuri, lakini haufuati utaratibu, sheria na kanuni ambazo imejiwekea.
Riziki haachi kueleza athari za mgogoro wa uongozi ndani ya CUF, anaoamini uliasisiwa na Profesa Ibrahim Lipumba, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, kwa msaada wa vyombo vya serikali, ikiwemo ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
“Mgogoro huu unatuathiri kiasi chake. Fedha za ruzuku zimezuiliwa kwa sababu ya suala hili. Wabunge na chama tunashindwa kuendesha shughuli za maendeleo katika majimbo ipasavyo. Tunalazimika kuchangishana mfukoni,” analalamika.
Riziki ni mtaalam wa Sayansi ya Siasa, elimu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ngazi ya Shahada mwaka 1982 hadi 1985. Pia ana Shahada ya Uzamili ya Masuala ya Kimataifa aliyoisomea katika Chuo Kikuu cha Colombia, Marekani.
Elimu ya sekondari alisoma shule ya wasichana Kisutu na elimu ya msingi aliipatia Shule ya Msingi Ilala Bungoni, Dar es Salaam mwaka 1967 hadi 1973.
Mwaka 1985/86 alifundisha Shule ya Sekondari ya Masjid Quba ya jijini Dar es Salaam. Riziki alifundisha masuala ya diplomasia mwaka 1986/2015 katika Chuo cha Diplomasia Kurasini Dar es Salaam, na baadhi ya aliowafundisha ni wabunge Nape Nnauye (Mtama), Marry Mwanjelwa (Viti Maalum) na Sixtus Mapunda (Mbinga Mjini).
TANBIHI: Makala hii iliyoandikwa na Pendo Omary ilichapishwa kwa mara ya kwanza na gazeti la MwanaHalisi katika toleo lake la tarehe 17 Julai 2017.