Showing posts with label uchunguzi. Show all posts
Showing posts with label uchunguzi. Show all posts

Monday, 5 September 2016


Kulia: Haruna Mbeyu, Sheikh Kondo Bungo na Mwandishi Masjid Kichangani
Magomeni Mapipa
Nimekutana na Sheikh Kondo Bungo Msikiti wa Kichangani Magomeni na kwa kipindi cha chini ya saa moja tuliposimama nje ya msikiti Mwalimu na Sheikh Kondo alinichukua safari ndefu yenye simulizi za kusisimua, kutisha na kusikitisha. Kuanzia kusakwa hadi kufikia kugombea ubunge Mbagala Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kuishia mahakamani kupigania ushindi wake anaosema umeporwa...

In Shaallah kesi yake itakapofikia tamati tutakiweka hapa kisa cha Sheikh Kondo Bungo kama atakavyoeleza kwa maneno yake mwenyewe. 

Hakika ni mchezo wa senema khasa inayovutia.

Friday, 2 September 2016

Utangulizi
Fuatilia ukurasa huu kuhusu taarifa za kuhojiwa na Polisi, Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso imam, sheikh na mwalimu wa chekechea na shule ya Msingi ya Kiislam, Mabawa Tanga na pia mwalimu wa kusomesha Maarifa ya Kiislam katika Shule za Sekondari pamoja na kuhojiwa Sheikh Salim Barahiyan Mudir wa Tanga Muslim Youth wamiliki wa shule, hospitali, Kituo cha Radio ya Kiislam na taasisi kadhaa zinazojishughulisha na maendeleo ya Uislam Tanzania...Na Bakari Mwakangwale

HOFU imetanda Jijini Tanga, kufuatia Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwahoji baadhi ya Masheikh maarufu na viongozi wa Taasisi za Kiislamu Jijini humo.

Miongoni mwa Masheikh waliofikishwa kituo Kikuu cha Polisi na kuhojiwa ni pamoja na Sheikh Salim Barahiyanina Ustadhi Chambuso  Ramadhani.

Hata hivyo haijajulikana wamehojiwa kwa tuhuma zipi, huku Amir wa Baraza la Vijana wa Kiislamu Tanzania, Ustadhi Ahmed Kidege, yeye ametuhumiwa kwa uchochezi.

Akizungumzia hali hiyo, kwa njia ya simu kutoka Jijini Tanga, Ustadhi Hamisi Shemtoi, alisema kumekuwa na taarifa kwa muda mrefu kwamba kuna baadhi ya Masheikh na viongozi wa dini wanatafutwa na Polisi.

Alisema, kufuatia taarifa hizo, Masheikh wamekuwa wakielezana kwamba, wajiandae kisaikolojia kwani wakati wowote wanaweza kukamatwa.

Akizungumzia kukamatwa Kwa Kiongozi wa Baraza la Vijana  wa Kiislamu Tanzania, Ust. Shemtoi, alisema Amir Kidege, alivamiwa na kumatwa na askari wanane, majira ya saa tano asubuhi Jumatatu wiki hii, akiwa ofisini kwake.

Alisema, baada ya kumatwa, aliwaomba maafande hao kutoa taarifa na kuruhusiwa ambapo alimpigia simu Ustadhi Shemtoi na kumeleza juu ya kukamatwa kwake na Polisi.

Alisema, baada ya kupokea taarifa hizo, ilimlazimu kwanza kuswali rakaa mbili za sunna, kwani alisema alifanya hivyo kumuomba Allah (sw) kutokana na hali ilivyo sasa kwani alijandaa kwa lolote dhidi yake katika ufuatiliaji huo.

Alisema, alishangaa baada ya kufika Polisi aliulizwa iwapo yeye ndiye Sheikh Chambuso, ambapo alijibu hapana, bali yeye ni Ustadhi Shemtoi, na kwamba amefika hapo kwa ajili ya kufuatilia kadhia ya kukamatwa kijana wake Ustadhi Ahmed Kidege.

Alisema, baada ya utambulisho huo, alikabidhiwa kwa Afande aliyejitambulisha kwamba ndiye kiongozi wa operesheni hiyo, na kwamba alielezwa kuwa wamemkamata kijana wake kwa ajili ya mahojiano ya kawaida, lakini kuna simu yake moja ameiacha ambayo inahitajika hapo Piolisi.

“Nililazimika kurudi hadi nyumbani kwake kuifuatilia hiyo simu ambayo alikuwa akiitumia ofisini kwake kisha niliisalimisha kwa kuwakabidhi.” Ameeleza Ustadhi Shemtoi.

Alisema, baada ya mahojiano na Polisi, walimwachia majira ya Magharibi, baada ya kumuwekea dhamana na kutakiwa kumrudisha siku ya Ijumaa (leo) majira ya saa mbili asubuhi kwa ajili ya kuripoti kituoni hapo.

Alisema, kwa mujibu wa fomu ya dhamana aliyojaza na kusaini imeonyesha kuwa anamdhamini Ustadhi Ahmed Kidege, kwa tuhuma za uchochezi.

“Lakini alipokuwa akihojiwa hawakumueleza kachochea nini, kamchochea nani wala eneo maalum alilotumia kuchochea, Msikitini, katika Kongamano au katika mitandao, lakini pamoja na yote hayo wamemwachia baada ya mahojiano ya masaa mawili.” Amesema Ust. Shemtoi.

Alisema, kikubwa wamechukua maelezo yake binafsi (CV) na kwa kuwa shughuli zake ni kufundisha mashuleni somo la Maarifa ya Uislamu (EDK), pia walitaka kujua analipwa na nani, ambapo aliwaeleza yeye anajitolea katika kazi hiyo.

Aidha, alisema wakati anaingia pale Kituo Kikuu cha Polisi, alikutana na Sheikh Salim Barahiyani, akiwa katika gari yake anatoka ambapo alimueleza kuwa anatoka ofisi za Uhamiaji, ambazo zipo hapo hapo Polisi.

Hata hivyo, badae kwa taarifa walizozipata ni kuwa Sheikh Barahiyani, alionekana tena hapo upande wa Polisi Makao Makuu, ambapo imeelezwa kuwa aliitwa kwa mahojiano na Jeshi la Polisi.

Alisema, mbali ya Sheikh Barahiyani, pia walikutana na Sheikh Chambuso Ramadhan, wakati yeye (Shemtoi) anapandisha akiwa na Ust. Kidege Ahmed, walimuona Sheikh Chambuso, akishushwa.

“Yeye hakukamatwa, alipigiwa simu akaenda mwenyewe na baada ya kuhojiwa wamezuia simu zake hapo Polisi.” Ameeleza Ust. Shemtoi.

Aidha, alisema Imamu wa Masjid Qubah, Barabara ya 15 Sokomjinga, Sheikh Ngaluba, naye alifuatwa na maafande wa Jeshi la Polisi, lakini hawakufanikwia kumkamata kwani hakuwepo katika eneo walilokusudia kumkamata.

Zaidi, alisema kwa siku ya Jumanne wiki hii amepata taarifa kuwa Amir wa Taasisi ya Dalur Hadith Ulumy,  ya Jijini humo Sheikh Ally Kiroboto, naye wamemkamata na kwenda kuhojiwa.

Imeelezwa kuwa hali hiyo imezidi kutia hofu wakazi wa Jiji la Tanga, wakizingatia kupotea kwa ndugu na jamaa zao katika mazingira ya kutatanisha, huku wakikosa taarifa kamili hata pale wanapokwenda katika vituo vya Polisi, Gerezani na hata katika Hospitali.

Kufatia matukio hayo, Jukwaa la Vijana wa Kiislamu Tanzania, limetoa tahadhari kwa Waislamu hususani vijana kuachana na mambo yanayotia shaka vyombo vya usalama, ikiwemo kutuma na kupokea jumbe (sms) zenye mashaka kupitia simu za mkono na mitandao ya kijamii.

  ***
Unaweza kusoma historia fupi ya Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso katika juhudi zake za malezi ya watoto wadogo na vijana na katika kusomesha Uislam katika Mkoa wa Tanga...
Ingia hapo chini:


Nilipofika Tanga mwaka wa 1997 nikapata hamu ya kusoma Uislam lau kwa uchache wa kusoma. Sheikh Salim Barahiyan siku ya kwanza nilipofika darsani kwake Msikiti wa Ansar Barabara ya 20 nilimkuta anasomesha ''Riadh-Us-Saleheen.'' Kitabu kikubwa sana kwangu lakini nitafanyaje basi nikajiunga na mimi katika darsa.

Baadae nikajaelezwa kuwa nilikuwa kivutio cha aina yake katika darsa lile kwanza kwa mavazi yangu ambayo ndiyo nilikuwa navaa ofisini kwa hiyo kwa kuwa sikuwa na muda wa kwenda nyumbani kubadili kwa kuchelea kuchelewa darsa nilikuwa nikendanazo darsani hivyo hivyo.

Kwa wengi nilionekana mtu mtanashati na mtu wa kujipenda. Lakini zaidi lililovutia ni gari langu la kisasa nililokuwa ninagesha nje ya msikiti. Taratibu nikazoeleka pale darsani si kwa wanafunzi wenzangu bali hata kwa sheikh mwenyewe mwalimu wetu Sheikh Salim.

Sheikh Salim yeye ni kiongozi wa Ansar na Ansar wana namna yao ya uvaaji na kujiweka. Ikiwa kivazi ni kanzu au suruali basi lazima iwe juu ya kifundo na kisha lazima ufuge ndevu lau kama ni chache.

Haya yote ni katika mafunzo na suna ya Mtume (SAW). Bahati mbaya sana mimi sikuwa hata na moja katika hayo. Sivai suruali juu ya kifundo wala sifugi ndevu.

Ikawa sasa Sheikh Salim baada ya kudarsisha kwa muda akihisi kama wanafunzi wake tumechoka yeye husimama kidogo na kufanya maskhara ili wanafunzi wake turudishe nguvu za kumsikiliza.

Hapo Sheikh atanifanyia maskahara atasema, ''Sheikh Mohamed naona hicho kidevu chako kimekuwa cheupe kama ''bulb,'' au yai vile.''

Basi darsa zima litageuka kunitazama na sote tutaangua kicheko...

Sheikh Salim alinipenda sana na akanitia kwenye Bodi ya Shule na alikuwa akituita katika vikao akitupa na posho.

Mimi nililalamika kuhusu hizi posho lakini akanituliza akanambia, ''Sheikh Mohamed hebu nisikize, nyie huko makazini kwenu vikao vyote mnavyohudhuria mnalipwa, iweje hiki za shughuli za Kiislam ndiyo tusikulipeni?'' Sheikh Salim hakutaka kusikiliza chochote kuhusu sisi kukataa kupokea posho.

Sheikh Salim Barahiyan kafanya mengi katika kuwahudumia Waislam wa Tanga inataka ufike kwanza uione ofisi yake kisha utembelee taasisi zilizokuwa chini ya Ansar ndipo utaelewa kazi kubwa aliyofanya msomi huyu mwenye shahada mbili za Sharia moja kutoka Saudia na nyingine Pakistan.

Mwandishi alipokuwa mwanafunzi wa Sheikh Salim Barahiyan Tanga katika
miaka ya mwishoni 1990

Thursday, 21 July 2016


Imewekwa picha ya Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NSSF Bi. Chiku Matesa na mwekaji ameandika maneno haya:

''...hahaaa huyu mama ndio afisa rasilimali pale NSSF ambaye alisimamishwa juzi kwa uchunguzi anaitwa Chiku, anatakiwa ahojiwe kisha afungwe ni kwa nini aliajiri vihiyo wengi hivyo??

Mwandishi katoa hukumu hata kesi bado kusikilizwa.
Mimi nikaja na majibu haya:Kibo,
Huko kuonewa kwa ajili ya dini si tatizo geni Tanzania wala hakuna Muislam atakaeshangazwa na hili.

Hamza Njozi aliandika haya katika kitabu chake, ''Mwembechai Killings..:''

''This book is about one old skeleton in our national cabinet; the burden of religious discrimination which we have always carried in our hearts but which we have carefully managed to conceal to the rest of the world. President Reagan of the United States once boasted about the global reach of his country by saying: You can run but you cannot hide. But as far as our religious skeleton is concerned, we have managed to fool even the arrogantly boastful America. All the official reports published by the US Department of State from 1994 to 1999 have failed to detect religious discrimination in Tanzania. The focus of this book is on the discrimination which Muslims suffer in their country. This does not mean that no one has suffered in Tanzania except the Muslims. To be sure, in their numerous writings, Issa G. Shivji and Chris Peter Maina have unearthed several sickening skeletons as far as our general record in respecting human rights is concerned. But it is the suffering of Muslims in Tanzania which has rarely been acknowledged even in our own country. Who can imagine, for example, that President Mkapa’s speech quoted above was delivered nine months after his government had ordered policemen to shoot and kill Muslims at Mwembechai? This book is offered as a modest attempt to understand the intricate weave of social and political factors which threaten our national unity.''

http://www.islamtanzania.org/mwembechai/mchai-chap1.pdf


Chinchilla...
Sasa ikiwa hivyo ndivyo na hili nalo liangaliwe:

''In public Mwalimu Nyerere was a fierce defender of secularism. It is therefore quite disturbing to learn that in private he championed the sectional interests of his own church. In 1970 Nyerere invited to the State House the then Secretary General of the Tanzania Episcopal Conference, Fr. Robert Rweyemamu and the Pope’s Representative to Tanzania Mgr. Giovano Cerrano. Among other things Nyerere told his guests that he was doing every thing in his power to strengthen Catholicism in the country. He also requested them to go and inform the Bishops that he had established a Department of Political Education in TANU (the ruling and only political party at that time), and that he had appointed a Christian Reverend to head that department, not because of his competence as a political analyst, but because of his strong faith as a Christian. His responsibility was to guide and control the political direction of the party. He also informed them that in the Party’s National Executive Committee (NEC) two members were Reverends. He said he believed that was the best way of ensuring that the party got good people(van Bergen, 1981:333-336).''
(Njozi 2002)

Chinchila...
Waislam hatuna hofu na mambo haya ya udini kwa kuwa hatujapatapo
kumdhulumu au kumbagua mtu kwa ajili ya dini yake.

Nyerere angelikuwa hai yeye angekuwa shahidi yetu.

Kapokelewa na Waislam kalala nyumba zao na kala nao chakula sahani
moja hadi akapata ukubwa wa nchi.

Hakuna aliyembagua kwa Ukatokili wake.

Rafiki zake wapenzi na vijana rika lake walikuwa Abdulwahid na Ally
Sykes 
na Dossa Aziz.

Kushoto; Dossa Aziz, Julius Nyerere Abdul Sykes na Lawi Sijaona
Wazee wake walikuwa Mshume Kiyate, Sheikh Suleiman Takadir na
Jumbe Tambaza kuwataja wachache.

Mshume Kiyate na Julius Nyerere 1964


Jumbe Tambaza

Kulia: Bi. Tatu biti Mzee, wa tatu Julius Nyerere wa tano Bi.Titi Mohamed 
wakimsindikiza Nyerere uwanja wa Ndege Dar es Salaam safari ya UNO 1955

Dada zake walikuwa Bi. Hawa biti Maftah, Tatu biti Mzee na Bi. Titi
Mohamed 
kwa kuwataja wachache.

Hii ndiyo historia ya Waislam.

Sisi hatuna hofu na uchunguzi wa wanaoleta udini kwani sisi ndiyo waathirika
wakuu.

Jaji...
Kuna kisa cha kuchekesha kidogo.

Kamati moja ya bunge ilikwenda kwenye taasisi moja ya serikali
kuchunguza tuhumu za udini za mkuregenzi Muislam.

Yule mkurugenzi Muislam akawauliza, ''Nyie mmekuja kunihoji mie
kwa tuhuma za udini sasa mbona nyie wote Wakristo watupu kwani
huko Bungeni hakuna Waislam?''


[​IMG]
Chinchilla...
Vipi na huyu anaetoa fedha za shirika la umma kujenga kanisa.
Mimi nahifadhi jina lake na taasisi yake.

Huyu hastahili na yeye kuhojiwa vipi anatoa mamilioni ya shirika
lake kulipa kanisa lake?

Naiomba Majlis ilitazame na hili.
Huu ndiyo uadilifu 1. Superuser,
  Hapana haja ya kunitukana ikiwa nimekosea hilo si shirika
  la umma nifahamishe tu ili nijue na mimi nitakushukuru kwa
  kunielimisha.

  [​IMG]

  Mtoaji akikabidhi hundi ya shs: 10,000,000.00 kwa kanisa la KKKT.
 2. M

  Mohamed SaidVerified User 

  #124
  33 minutes ago
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 8,226
   
  Likes Received: 1,622
   
  Trophy Points: 280

Lukesam,
Ikiwa utahitaji mimi nikupe ushahidi wa kimahakama sitoweza labda hili
jambo lende mahakamani.

Ninaloweza kuonyesha hapa ni ushahidi wa yanayoandikwa na wahusika
wenyewe.

Ingia hapa:
http://www.tanzaniatoday.co.tz/news/benki-ya-crdb-yachangia-milioni-20-ujenzi-wa-kanisa-la-kkkt-jimbo-la-haiBabu...
Nataka nikuunge mkono kwa kukuwekea nukuu kutoka kwa Njozi (2002):

''The church was particularly worried by the unity and organisational capacity of Muslims under the East African Muslim Welfare Society (1992:35-37). Because the church said the EAMWS was dangerous in that it would weaken Christianity, it had to be so. Mwalimu Nyerere used his political powers to ban this legitimate organisation, to confiscate all its properties and to impose on the Muslims a puppet organisation, BAKWATA. As its name suggests, the EAMWS was a welfare organisation whose primary objective was to provide education and health services. The intellectual brilliance of Mwalimu Nyerere is well-known, and so is his sense of social justice. But Nyerere was also a sincere Roman Catholic. He could not pick and choose what to follow and what to reject in his faith.''

Saturday, 2 July 2016


Wanamajlis,
Nimepokea taarifa hii leo asubuhi najaribu kupata ukweli:

[11:11am, 02/07/2016 WAISLAM WAKATALIWA KUTUMIA UWANJA WA UHURU KWENYE SHEREHE ZA EID.

*MWANZO WALIKUBALIWA NA WAKAAMBIWA WALIPIE Tsh 10,000,000/=

*BAADA YA KUTEKELEZA MAELEKEZO HAYO , IKAJA AMRI NYINGINE YA KUNYIMWA KIBALI CHA MATUMIZI YA UWANJA HUO.

*WAISLAM WATILIA SHAKA KUWA KUNA AGENDA YA SIRI, KWANI HAKUKUWA NA SABABU ZA MSINGI.

*WAISLAM WAOMBA RAIS KUINGILIA KATI.

* YATANGAAZWA KUPATIKANA KWA HASARA YA ZAIDI TSH. 50,000,000/= KWAJILI MAANDALIZI YA SHEREHE HIZO.


[​IMG]
Mashindano ya kuhifadhi Qur'an Uwanja wa Uhuru yaliyotayarishwa na
Sheikh Nurdin Kishki Mwezi wa Ramadhani 2016
Mashindano yakuhifadhi Qur'an yalijaza watu kushinda mpira katika uwanja ule...ujumbe ule ni mzito kwani dunia nzima picha za Waislam walioshonana kusikiza Qur'an zilionekana...wengi bila shaka walisema, "Ala Tanzania kumbe Waislam wengi vile!" Hii inawezekana imewatisha wenye mamlaka ya kutoa na kutotoa, wenye mamlaka ya kuwasha na kuzima...

Ukiitazama hiyo picha unaweza kudhania Simba na Yanga wako uwanjani wanawania kombe la ubingwa lakini siyo umma umekuja kusikiliza Qur'an siyo kuangalia mpira.

Hii haijapatapo kutokea nchini petu.
Alhamdulilah...


Photo


Photo

Photo


Thursday, 30 June 2016


Carlos...
Mijadala hii inahitaji ustahamilivu sana kwa kuwa wengi wanaokuja
kuchangia huwa wanakuja wakiwa tayari wameshaathirika sana na
historia ya aina ya Chuo Cha Kivukoni.

Anapoelezwa historia ambayo inapingana na ile na khasa anaposoma
majina ya Waislam hamaki zinampanda na kuanza kwa kweli wakati
mwingine kutoa hata matusi.

Lakni mimi najua kuwa hayo ninayomueleza ndiyo kweli yenyewe hata
kama kwake ndiyo mara ya kwanza kaisikia.

Hapo inataka utaratibu na jambo lolote likitanguliwa na upole jambo
hupendeza.

Kuna mtu kaja hapa barzani ananidai mimi nimpe data za shule ngapi
Waislam wanazo.

Yeye anataka hizo data ili afananishe na takwimu za vyuo ambavyo
Kanisa limejenga.

Yeye anajuna wazi na fika kuwa Waislam mayatima hawana lolote la
kuonyesha.

Nikamwambia ukitaka kujua tatizo hili tusianze na data kutoka kwa
Waislam tuanze na data kutoka vyanzo vya kanisa vipi limeweza kuwa
kama lilivyo Tanzania.

Nikawa nampa rejea za kusoma.

Akawa anajibu kwa kejeli na kibri na kusoma hizo rejea hataki na hapo
nilimtahadharisha uzito wa hilo somo.

Lakini mimi sikuwa na haraka na yeye kwani najua wapi utakuwa ukomo
wake.

Katika kujibu maswali ya wachangiaji wengine waliotaka kujua kulikoni na
mimi nikawa najibu sasa yeye akaanza kuelewa kuwa lipo jambo kwani
serikali yenyewe ilipiga marufuku kitabu cha Hamza Njozi, ''Mwembechai
Killings...'' baada ya kuja na ushahidi ambao Mkapa aliudai kutoka kwa
Waislam kuwa ipo dhulma.

Mkapa alipoingia madarakani aliomba apewe ''ushahidi wa kisayansi,''
kutoka kwa Waislam kuwa katika serikali kuna watu wanatumia nafasi
zao kuwakandamiza Waislam.

Hii ilikuwa Ukumbi wa Diamond akijibu hotuba ya Islamic Club iliyosomwa na
Ramadhani Madabida.

Usia wangu kwenu nyote ni kuwa tusiache kueleza ukweli taratibu hili jambo
litaeleweka.

Katika kueleweka hili tatizo dawa yake In Shaallah itapatikana.

[​IMG]
Prof. Njozi na Mwandishi Johannesburg 2006

Wednesday, 18 May 2016


Bunge la Bajeti Wizara ya Mambo ya Ndani Mheshimiwa Riziki Shahari Mbunge wa Mafia Viti Maalum CUF alipoihoji serikali kuhusu hatima ya masheikh waliowekwa gerezani kwa tuhuma za ugaidi. Ingia hapo chini:
Photo
Picha ya juu Mh. Riziki Shahari akiwa na wabunge wenzake wakitoka nje ya Bunge

Photo
Mh. Riziki Shahari Mngwali
Columbia, New York


Sunday, 17 April 2016

Masopakyindi,
Umetia wasiwasi ambao hauna sababu.
Kwanza si mimi niliyeliita daraja hilo Daraja la Dau.

Jina hilo nimelipata Kariakoo.

Kila yanapokuja mazungumzo ya Dau basi likitajwa daraja 
wataliita Daraja la Dau.

Mfano wa Rais Magufuli na Dau hauendani katika hili.
Rais Magufuli ni mkubwa wa nchi nzima.

Dr. Dau yeye alikuwa mkurugenzi tu wa taasisi iliyojenga
daraja.

Sasa kwa watu wa Dar es Salaam na khasa ukimchukulia
Dr. Dau alivyokuwa na mkabala na hawa nduguze kila lake
wao huliona lao.

Hii ndiyo sababu nadhani wakaliita daraja lile Daraja la Dau.

Hata mie siku nilipomwambia kuwa daraja linaitwa Dau yeye
alicheka.

Na unajua Dau kakulia Kariakoo utoto akicheza mpira Yanga
Kids na akina Tostao, Adolf Rishad na Kassim Manara na
hii imeongeza sana umaarufu wake hapa mjini.

Na umaarufu una bei yake.
Moja ni kama hili tunaloliongea hapa.

Najua fika kuna watu watakasirika wakisikia daraja linanasibishwa
na Dr. Dau.

Lakini tuna la kufanya kuzuia mapenzi ya watu?

Wanangu wananiuliza, ''Baba lini tutakwenda kuliona daraja la Uncle
Dau
?''

Lakini haya ni ya kupita.

Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika kuna sheikh mkubwa sana
katika TANU akihutubia wanachama wa TANU katika taarab Mtaa wa 
Mvita kwenye tawi lililokuwa na nguvu kushinda matawi yote Tanganyika
alimwita Mwalimu Nyerere, ''Mtume wa Afrika.''

Wana TANU wenyewe waliona sheikh sasa kavuka mpaka na hili lilileta
farka kubwa sana ndani na nje ya uongozi wa TANU.

Mapenzi yakizidi yana khatari zake.
Dr. Dau ni mhanga wa watu wa Dar es Salaam kumpenda sana.